Moja ya taarifa mbaya iliyonifikia Asubuhi ya leo July 6, 2017 ni msiba wa Mwanamuziki mkongwe wa Band ya Msondo Ngoma Shaaban Dede, ambaye amefariki dunia akiwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
Mtoto wa marehemu Hamad Dede amethibitisha kifo cha Shaaban Dede akisema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala, DSM na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara baada ya kukamilika.