Latest Updates

Diamond Afichua Sababu ya Zari Kumsamehe Baada ya Kuchepuka na Kuzaa na Hamisa Mobeto


Baada ya mwanamuziki Diamond Platnuzm kukiri hadharani kuwa alichepuka na Hamisa Mobeto na kuzaa nae, wengi waliamini kwamba huo ndio ulikuwa mwisho wa uhusiano wake na Zari kwani mara kadhaa amekuwa akikanusha kwamba hakuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Hamisa, kumbe ni uongo.

Tetesi za kuwa Diamond na Zari wameachana zilizidi kushika kasi baada ya mwanadada huyo kutokea Uganda kufuta picha zote zenye sura ya Diamond katika ukurasa wake wa Instagram, kutohudhuria sherehe yake ya kuzaliwa, na wala kutomtumia ujumbe katika siku yake ya kuzaliwa kama anavyofanya mara nyingine.

Lakini ukweli ni kwamba wawili hao bado wapo pamoja, na kwamba maisha yao yanaendelea, huku wengi wakimsifu Zari kwa moyo wake wa kijasiri namna anavyoweza kuvumilia masuala ambayo yanawatesa wengi katika uhusiano.

Licha ya kuwa wengi hawajui Diamond alitumia njia gani kuomba msamaha hadi mzazi mwenzake huyo waliyezaa naye watoto wawili akamsamehe, ameamua kuweka hadharani, mbinu zake za kivita zilizomsaidia kupata ushindi na kutoka kifua mbele.

Diamond amesema kuwa, baada ya kuona mambo yanakuwa mabaya na kwamba karibia atamkosa Zari, aliamua kukwea pipa (ndegep) hadi Afrika Kusini kwenda kuyamaliza na mrembo huyo.

Aliyasema hyo jana usiku wakati anatumbuzi katika tamasha la muziki lililofanyika Zanzibar ambapo alikuwa pamoja na mrembo huyo aliyekuja nchini kwa shughuli nyingine za kibishara.

“Unajua hapa katika palitokea mambo mambo mengi, Shetani akaingia katikati, mara hooo hivi na vile, mambo yakawa mengi kweli, nikaona eehe mtoto wa kiganda kacharuka,” alisema.

Diamond aliendelea kuwaambia mashabiki zake waliokuwa wakishangilia, “Nikiangalia kushoto na kulia nikaona kabisa jiko naelekea kulikosa moja kwa moja, nikakwea pipa nikaruka kwenda south (Afrika Kusini).”

Alisema kuwa baada ya kufika Afrika Kusini, kabla hajaongea kitu chochote aliingia hadi chumbani, kisha akafanya vitu vingi sana akiwa humo chumbani vilivyosaidia akasamehewa.

Zari alipokuja nchini alikanusha kuwa amekuja kwa ajili ya Diamond na kusema amekuja kwa shughuli zake za kibiashara wakitu huo, Diamond alikuwa nje ya nchi kwa masuala ya muziki, lakini wawili hao walikwenda wote Zanzibar jana mchana.