Latest Updates

Ziliendwa Yazidi Kuwagharimu WCB, Sasa watakiwa Kuilipa Msondo Ngoma Milioni 300




Bend kongwe ya Muziki wa Dansi Nchini Msondo Ngoma ikimtumia Maxim Advocates imeweza Kudai Kiasi cha Tsh Milioni 300 kwa Lebo inayomilikiwa na Diamond Platnumz kwa kile walichodai kuwa kutumiwa Ala yake ya muziki katika wimbo wa “Zilipendwa” ambao unamilikiwa na wasanii wa Lebo hiyo ya WCB Wasafi.

Katika Document waliyoandikiwa WCB inaonyesha kuwa kionjo kilichotumika cha Tarumbeta kilishawahi kutumika katika moja ya nyimbo za Bendi ya Msondo Ngoma kupitia wimbo wao wa “Ajali”.

WCB Wasafi wametakiwa Kulipa kiasi hicho cha Pesa Ndani ya Siku Saba la Sivyo watafikishwa Mahakamani.